Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, Tundu Lissu walipokuwa kwenye kikao cha Bunge hivi karibuni ribuni.
Picha na Mkataba
Habari kutoka vyanjo mbalimbali hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa
rasmi uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Baada
ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo kutupilia mbali kesi
iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo
(Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama wake ndani ya chama hicho…
Habari
zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Akitangaza
hatua hiyo ya kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za chama hicho
ziko wazi na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho
mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama. Source
from Mwananchi News.By Kimena nuhu.