Timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam, leo
imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga SC baada ya kuifunga goli 1-0 goli lililowekwa
kimiani na mshambuliaji Emmanuel Okwi katika dakika ya 53 kipindi cha pili.Hali
hiyo imesababisha baadhi ya mashabiki wa yanga waliko AMUCTA Tabora kufunga
simu zao.
Mechi hiyo ya ligi kuu imefanyika katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam ikuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka katika
pande zote za timu hizo waliofurika kwa wingi uwanjani hapo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro akisaidiwa na
Souda Lila wa Dar pamoja na Florent Zablon wa Dodoma ulimalizika
kwa kiongo wa Yanga Haruna Niyonzima kuzawadiwa kadi nyekundu baada ya
kuonyeshwa kadi mbili za njano.
By Kimena Nuhu